Nenda kwa yaliyomo

Chari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto wa Chari
Mto Chari
Mdomo Ziwa Chad
Nchi Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kamerun
Urefu 1,200 km
Kimo cha chanzo 500 - 600 m
Mkondo ??
Eneo la beseni 669,706 km²

Chari (Shari) ni mto mkubwa unaoishia katika Ziwa Chad. Unaanza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ukielekea kaskazini na kuingia nchi ya Chad. Baada ya kupita mji mkuu N'Djamena mto huu unaunda mpaka na Kamerun halafu unaishia katika Ziwa Chad.

Chari unatiririsha 90% ya maji yote ya kuingia ziwa Chad. Hii inafanya mto huo kuwa chanzo kikuu cha uhai wa Ziwa Chad na mfumo wake wa ekolojia.

Idadi kubwa ya wakazi wa nchi ya Chad wanaishi karibu na mto, wakiwa pamoja na wale wa mji mkuu. Watu hao hutegemea mto kwa kilimo cha umwagiliaji, kwa uvuvi, hasa wa samaki aina ya sangara, na kwa matumizi ya maji nyumbani.

Wavuvi kwenye mto Chari.

Tawimto muhimu zaidi ni mto Logone, mengine ni Bahr Salamat, Bahr Sarh, Bahr Aouk na Bahr Keïta.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chari kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.