Dima Bilan

Dima Nikolayevich Bilan (anajulikana pia kama Viktor Nikolayevich Belan. Alizaliwa mnamo 24 Desemba 1981)[1] ni mwimbaji wa Urusi. Mnamo mwaka 2002, Bilan alishiriki katika msimu wa kwanza wa shindano la New Wave. Mwishoni mwa shindano hilo, alimaliza katika nafasi ya nne. Aliiwakilisha Urusi katika Shindano la Muziki la Eurovision mnamo mwaka 2006 na wimbo 'Never Let You Go' akishika nafasi ya pili, na alishinda shindano hilo mnamo mwaka 2008 huko Belgrade, kwa wimbo 'Believe'. [2][3][4]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Dima Bilan alizaliwa kama Viktor Belan huko Ust-Dzheguta katika jamhuri inayojitawala ya Karachay-Cherkessia, kwenye familia mchanganyiko yenye asili ya Kitatari, Kikarachay, na Kirusi. Baba yake Bilan, Nikolai Mikhailovich Belan, alizaliwa Kabardino-Balkaria na mama yake, Nina Dmitriyevna Belan, alizaliwa Tatarstan. Ana dada yake mkubwa anayeitwa Yelena, na mdogo wake wa kike anayeitwa Anna. Baada ya kuishi kwa muda mfupi huko Tatarstan akiwa mtoto, familia ya Bilan ilihamia Maysky huko Kabardino-Balkaria. [5][6]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Bilan alianza kazi yake ya muziki akiwa bado shuleni. Alikuwa akitumbuiza mara kwa mara kwenye sherehe za shule na mbele ya wageni nyumbani kwao. Katika miaka ya ujana wake, aliwaona Valeriy na Konstantin Meladze kama kielelezo chake . Mnamo mwaka 1995, alitumbuiza kwa mara ya kwanza kwenye shindano la muziki lililorushwa kwenye televisheni, akiimba wimbo wa Valeriy Meladze uitwao 'Aktrisa'. Wimbo wa Meladze wa mwaka 1997 uitwao 'Vera' ukawa wa muhimu sana kwa Bilan.[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://ria.ru/20090730/179160935.html
- ↑ https://24smi.org/celebrity/21-dima-bilan.html
- ↑ https://www.stav.kp.ru/daily/27249/4378688/
- ↑ https://nvsc.fandom.com/wiki/Dima_Bilan
- ↑ https://www.vesti.ru/article/2220817
- ↑ https://esctoday.com/10861/russia_the_story_behind_dima_bilans_believe/
- ↑ https://www.eurovision.com/eurovision-song-contest/belgrade-2008/participants/dima-bilan/
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dima Bilan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |