Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Kupatwa kwa Mwezi(kwa Kiingereza: lunar eclipse) ni hali ya Mwezi kutoonekana kwa sehemu au kabisa kwa muda hadi kuonekana tena kama mwezi mpevu. Badiliko hili linaweza kudumu saamoja hadi nne. Hali inayopelekea kupatwa kwa mwezi kunasababishwa na kivuli cha Dunia kinachomwaga giza juu ya Mwezi kabisa au kwa sehemu. Hali hii inatokea wakati Mwezi - Dunia na Jua zinakaa katika mstari mmoja, Dunia ikiwa katikati ya Jua na Mwezi. Hapo kivuli cha Dunia inafunika Mwezi. Inatokea tu wakati wa mwezi mpevu. ►Soma zaidi
Picha nzuri ya wiki
Marcus Garvey, 1924
Marcus Garvey (1887–1940) alikuwa mwanaharakati, mwandishi na msemaji wa kisiasa kutoka Jamaika, anayejulikana kama mmoja wa waanzilishi mashuhuri wa vuguvugu la Pan-Africanism. Kupitia Universal Negro Improvement Association (UNIA), alihamasisha umoja, kujitegemea kiuchumi na kisiasa, pamoja na kuimarishwa kwa fahari na utambulisho wa watu wenye asili ya Afrika duniani. Mawazo yake yalikuwa na ushawishi mkubwa katika harakati za baadaye za ukombozi na haki za watu weusi.
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 125,702
Idadi ya kurasa zote: 236,358 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Katika mwezi wa Agosti 2025 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 7.79 hivi, ambayo ni sawa na mara 251,607 kwa siku au mara 10,483 kila saa ambalo ni ongezeko la mara 4.5 ukilinganisha na mwaka 2024 mwezi wa Agosti. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.